Marekani imemuwekea vikwazo kamanda wa Kikosi cha Dharura nchini Sudan RSF Jenerali Hamdan Dagalo kutokana na vitendo vyake vya kusababisha machafuko na ukiukwaji wa haki za binaadamu uliofanywa na wanajeshi wake katika mzozo baina yao na jeshi la Sudan.
Taarifa ya wizara ya fedha ya Marekani imesema imemuwekea vikwazo kamanda huyo anayeongoza kikosi cha RSF kwa tuhuma za kuongoza kundi la wanajeshi wanaohusika na mauaji ya raia, mauaji ya kikabila na unyanyasaji wa kijinsia.
Kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa siku ya jana, chini ya vikwazo hivyo watazuia mali na vitu vyote vya Marekani vinavyomilikiwa na Dagalo.