ZINAZOVUMA:

Makubaliano kusitisha mzozo, muda waongezwa Sudan

Makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Sudan yanatakiwa kuendelea kwa siku...

Share na:

Marekani na Saudi Arabia zimeafiki kurefushwa kwa makubaliano ya muda wa kusitisha mapigano kati ya pande zinazozohasimiana nchini Sudan kwa siku nyingine tano.

Serikali za Washington na Riyadh zimetangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki moja zaidi.

Katika taarifa yao ya pamoja, wamekiri kwamba usitishaji wa mapigano haujazingatiwa kikamilifu, lakini wanasema umeruhusu kufikishwa kwa misaada kwa watu milioni mbili nchini Sudan.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani lilisema kuwa hali ya utulivu katika mapigano iliiruhusu kutuma vifaa kwa wakazi waliokwama katika mji mkuu, Khartoum, kwa mara ya kwanza tangu mapigano yalipozuka wiki sita zilizopita.

Jeshi la Sudan na wapinzani wake kutoka kikosi cha dharura wameshutumiana kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya usitishaji mapigano, hasa katika eneo la Darfur.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya