ZINAZOVUMA:

Uteuzi wa balozi Dkt.Nchimbi kuwa katibu mkuu mpya CCM kwa hakika CCM ni bweta la viongozi mahiri

Uchambuzi wa Maeneo ma 3 muhimu ya Kitajriba katika uteuzi...

Share na:

Anaandikia Dkt. Ahmed Sovu

Tarehe 15/Januari/2024 Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan iliketi, pamoja na mambo mengine iliridhia uteuzi wa kamati kuu wa kumteua Mheshimiwa Balozi (Mstf) Daktari Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu mkuu wa 12 wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Uteuzi huu tunaweza kusema umekuja wakati mwafaka. Na hii imedhihirisha kuwa CCM ni Bweta (Shubaka) hazina ya viongozi mahiri.

Uteuzi huu ni muhimu kwa sasa na umekuja wakati adhimu sana na kutokana na tajriba ya Mheshimiwa Daktari Nchimbi. Daktari Nchimbi ana uzoefu katika maeneo matatu muhimu sana.

Fuatilia …👇👇

Eneo la kwanza – Ki chama

Dkt.Nchimbi si mgeni hata kidogo katika Chama cha CCM. Anakijua chama vilivyo na amewahi kushika nyadhifa kadhaa ndani ya chama, ikiwamo nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa. Tajiriba yake adhimu katika chama itasaidia kutekeleza majukumu yake ipasavyo hasa ukizingatia chama chake kinakabiliwa na shughuli ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mapema mwaka huu.

Unaweza kusema kama ni upere basi hapa umepata mkunaji. Kama ni shairi basi ndiye Malenga musharafu lau kama ni ngoma basi imempata manju mutribu.

Eneo la Pili – Kiserikali

Tajriba nyingine kubwa aliyonayo Daktari Nchimbi ni katika shughuli za serikali.

Historia inaonesha kuwa amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali. Amewahi kuwa mkuu wa Wilaya ya Bunda, amewahi kushika nyadhifa za uwaziri kama Naibu Waziri wa ulinzi na JKT, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, pia Wizara ya Ulinzi.

Amewahi kuwa Mbunge wa Songea Mjini. Kwa hakika katika shughuli za Dola ana tajriba kubwa. Akiwa Mtendaji mkuu wa Chama, tajriba hii ya kiserikali itamuwezesha kusimamia ilani ya chama chake ipasavyo. Mipito ya ki wizara inaijuia vema ni dhahiri ataongeza tija kubwa katika kuleta maendeleo yatakiwayo kwa Watanzania.

Eneo la Tatu- Kidiplomasia

Mheshimiwa Balozi Daktari Nchimbi ni Balozi Mstaafu. Ameshika wadhifa huo kwa miaka kadhaa. Amewahi kuhudumu kituo cha Ubalozi nchini Brazili na baadaye Misri.

Ni dhahiri CCM imempata mtu mwafaka anayeweza kujenga uhusiano na utangamano wa wanachama, viongozi na hata vyama rafiki vyenye usuhuba na muwasala na chama cha CCM.

Vilevile, uzoefu wake wa Kibalozi utasaidia kuchochea na kusimamia vilivyo, sera na falsafa ya Rais ya Dkt.Samia ya Diplomasia ya Kiuchumi. Pasipo shaka kuwapo kwake sera zaidi madhubuti zitaandaliwa kufikia malengo yao.

Ama kwa hakika, CCM ni hazina, CCM ni bweta la viongozi. Washindani wa CCM wakae mkao wa kula, wajipange na wajizatiti ipasavyo.

Mana CCM imesheheni, juu Mama la Mama, Mwenyekiti Dkt.Samia Suluhu Hassan, Makamu Mzee Komredi Abdurahman Kinana, Katibu Mwanadiplomasia Balozi Dkt.Nchimbi chini hapa mwamba, mzee wa Farasi Mheshimiwa Paul Makonda 🤣🤣 Mwenezi Shughuli ipo.

Kongoleni sana CCM kwa kuendelea kupanga safu madhubuti ya CCM. Uteuzi huu wa Dkt.Nchimbi umethibitisha kuwa CCM kwa hakika ni Bweta la uongozi.

Ushauri wetu kwa ujumla ni kuwa;

  • Ataendelea kuwaunganisha wana CCM wa ngazi zote.
  • Ataendelea kusimamia kanuni na miongozo na miiko yote ya CCM
  • Ataongeza vionjo vya kiubunifu katika utekelezaji wa majukumu yake
  • Ataendelea kusimamia falsafa ya R4 ya Dkt.Samia Suluhu Hassan
  • Atakiimarisha chama, mashinani, kwa mabalozi, katani kwa kufanya ziara na mafunzo mbalimbali n.k.
  • Wana CCM kumuunga mkono na kumpa ushirikiano wa dhati ili aweze kutimiza majukumu yake vilivyo.

Kongole sana Dkt.Nchimbi kwa kupokea kijiti hiki kwa mwamba Chongolo. Twakutakia kazi njema. Kama Wasemavyo CCM wenyewe; CCM IMEKAMILIKA, WACHA KAZI IENDELEEE.

Endelea Kusoma

Hamna chembe ya shaka katika hili, kwani tumejionea tangu kuanza kwa mashindano

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya