Anaaandika Dkt.Ahmad Sovu
Ni kama sikuamini macho yangu, kwa mandhari sharifu ya uwanja mpya wa Amaan ulioboreshwa. Kiwanja cha kisasa, skrini kubwa, vyumba vya kisasa vya wachezaji, viti vizuri vya kisasa hakuna wasiwasi wa mvua wala jua🤣🤣 aah! Kwa hakika Dkt.Mwinyi apewe maua yake tu💐.
Jana tarehe 27/12/2024 naweza kusema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amefunga mwaka kibabe katika sekta ya Michezo Zanzibar. Ambapo ameuzindua rasmi Uwanja mpya wa Amaan ulioboreshwa.
Wakati tunaandika makala haya, Nikakumbuka kaulimbiu yake inenayo; yajayo yanafurahisha, yajayo ni neema tupu
Kwa hakika neema katika sekta ya michezo na burudani imedhihirika na itakuwa na faida lukuki kwa Wazanzibar.
Faida za Ukarabati huo
Kwa hakika hatua hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya soka visiwani Zanzibar kwani;
- Itachochea kukua zaidi kwa soka na michezo mengine Zanzibar na Tanzania kwa jumla.
- Itaongeza fursa za kiuchumi na biashara. Kwa ubora wa uwanja ni dhahiri kwa sasa michezo ya mashindano mbalimbali itafanyika hapo hivyo kukuza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar.
- Itaongeza hali ya ulinzi na usalama. Kuwapo kwa mandhari ya uwanja kutafanya mazingira ya uwanjani na hata nje ya uwanja kuwa tulivu na kufanya watazamaji wakati wote wawe na furaha.
- Itasaidia kuibua vipaji zaidi na kuiongezea umuhimu sekta ya michezo kwa vijana na jamii kwa jumla.
- Itaongeza chachu ya kufanya vema zaidi kwa timu za Zanzibar katika mashindano ya ndani na nje.n.k
Neema zimekwisha?
Hapana bado yajayo yanafurahisha? Naam kwani katika uzinduzi alisema; “…Ninachoweza kuwaambia leo hapa,kumbe hawatujui? Sie hatujamaliza leo ndio tumeanza, huu kwetu sisi ni Ukarabati tu, kuuweka uwanja wa Amani katika mazingira safi, mazingira mazuri lakini bado kuna kitu kinakuja, hakijawahi kutokea … shangwe.”
Kauli hii ya Dkt.Mwinyi inaendelea kudhihirisha kuwa bado serikali yake ina dhamira kabambe ya kuendeleza soka la michezo kwa Zanzibar.
Ambapo alibainisha maeneo hayo kuwa ni;
- Kujenga uwanja mwingine wenye hadhi ya juu zaidi.
- Kuendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya michezo kwa kila wilaya kwa viwanja vipya vya kisasa.
- Vilevile Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ujerumani kupitia shirika la maendeleo GIZ imefunga mkataba wa makubaliano kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vitano vya michezo midogomidogo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa wavu , mpira wa mikono na mpira wa pete.
- Viwanja hivyo vinatarajiwa kujengwa Kangani Wilaya ya Mkoani, Mchangamdogo Wilaya ya Wete, Tumbatu na Mkokotoni Wilaya ya Kaskazini A na Haile Selasie Wilaya ya Mjini pamoja na viwanja vitatu vya Tennis Chakechake, Chuo kikuu cha SUZA Kampasi ya Nkurumah na Skuli ya Regeza Mwendo katika Wilaya ya Magharibi B.
- Vilevile, Serikali ya Dkt.Mwinyi imefanikiwa kuwapeleka vijana katika nchi mbalimbali ikiwamo Uturuki na Afrika Kusini kwa lengo la kuendelezwa na baadaye kucheza soka la kulipwa.
Huyu, ndio Rais Dk.Mwinyi kwa hakika anastahili kupewa maua yake.
Kwa hakika Dkt.Mwinyi na wasaidizi wake Mheshimiwa Tabia Mwita Waziri na viongozi wote wa Wizarani akiwamo Katibu mkuu Bi.Fatma Hamad kwa usaidizi ulotukua katika sekta ya Habari, Michezo na Sanaa.👏👏👏.