Katika uteuzi na kuhamishwa kwa viongozi mbalimbali, Mama samia amemuhamisha shirika maharage Chande.
Maharage Chande aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, amehamishiwa TTCL, na kuchukua nafasi ya Mhandisi Peter Ulanga.
Huku Mhandisi Gissima Nyamo Hanga kuwa mkurugenzi wa TANESCO, na kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Chande.
Mhandisi Gissima aliwahi kuwa Mkurugenzi wa REA (2008- 2019), na ni mkurugenzi wa bodi ya NICOL tangu mwaka 2022.
Mbali na kuhamishwa kwa Chande, pia Rais Samia amemteua mwenyekiti mwingine wa Bodi ya wakurugenzi ya TANESCO. Ambapo mwenyekiti mpya Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli amechukua nafasi ya Omar Issa.
Baada ya teuzi huu, Bw. Omar Issa ataendelea na majukumu yake aliyopangiwa na Tume ya Mipango iliyopo chini ya ofisi ya Rais. Omar Issa aliteuliwa katika bodi hiyo mwaka 2021, wakati wa Mhe. January Makamba kama Waziri wa Nishati.