Mlipuko mkubwa umetokea jirani na makao makuu ya Bunge katika mji mkuu wa Ankara nchini Uturuki ambapo Bunge likitarajiwa kufungua kikao cha shughuli zake, shirika la habari la AFP limeripoti.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uturuki imesema ni shambulio hilo ni shambulio la kigaidi lililofanywa na watu wawili.
“Magaidi wawili walionekana kwenye gari mbele ya lango la kuingilia la Kurugenzi Kuu ya Usalama ya Wizara yetu ya Mambo ya Ndani na kutekeleza shambulio la bomu”, imesema wizara hiyo.
Aidha Wizara hiyo imebainisha kuwa mlipuko huo umejeruhi maafisa wawili wa polisi, kulingana na uchunguzi wa awali uliofanyika.
Kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki, milio ya risasi pia ilisikika katika eneo yanapopatikana makao makuu ya Bunge na Wizara nyingi za nchi hiyo.