Serikali ya Brazil imetangaza vifo vya watu 11 kutokana na kimbunga katika jimbo la kusini mwa nchi hiyo la Rio Grande do Sul. Kimbunga hicho kimepita katika mji huo siku ya ijumaa na kuathiri miji mbalimbali ikiwemo miji ya Sao Leopoldo, Maquine pamoja na mji wa Caraa wenye wakazi zaidi ya 8,000 ambao umeathirika zaidi.
Dhoruba hiyo iliambatana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko maeneo mbalimbali. Mbali na idadi hiyo ya waliofariki pia wengine watu 20 wamepotea na msako umeendelea maeneo yaliyofurika.
Taarifa kutoka katika mamlaka zinasema, hadi kufikia Ijumaa usiku, Maquine, manispaa ya pwani ya mashariki, ilikuwa imepokea takriban futi moja ya mvua. Taarifa zaidi zimesema kuwa pamoja na hali hiyo kuwatia wasiwasi ila maeneo kama mji wa Caraa unawatia wasiwasi zaidi kwa kuwa unawahitaji wengi zaidi kutokana na wakazi wa mji huo.
Eduardo Leite, Gavana wa Jimbo la Rio Grande do sul amesema kuwa wameshafanya uokoaji wa watu 2400 ndani ya siku mbili na wahanga wengi wamejihifadhi katika viwanja vya michezo vya nje.
Bwana Leite amesema hayo alipotembelea wahanga katika moja ya maeneo waliyojihifadhi, na kuongeza kuwa lengo lao ni kuhifadhi na kuokoa maisha ya watupamoja na kutoa msaada ya kujikumu kwa familia zilizopatwa na janga hilo.