ZINAZOVUMA:

Korea Kaskazini kuzindua Gari mpya ya kivita

Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amehudhuria uzinduzi wa...

Share na:

Korea Kaskazini imezindua gari mpya ya kuangamiza vifaru, wakati wa ziara ya Rais Kim hivi majuzi katika Chuo cha Sayansi ya Ulinzi nchini humo.

Kifaa hicho kimetengenezwa na wachina na kina muundo wa kifaru chenye magurudumu 8 zinazotembea zote, kina uwezo wa kubeba watu 8.

Gari hiyo ina bunduki kuu ya milimita 105, bunduki ya pembeni ya milimita 12.7, na bunduki nyingine ya ya 7.62mm inayojitegemea.

Kifaa hiki cha kijeshi mahsusi kwa kupambana na vifaru kimeundwa ili kuongeza nguvu ya kijeshi na wepesi wa kusafirisha vikosi vya Korea Kaskazini kwa haraka, ili kuboresha ufanisi wa mapigano.

Kuzinduliwa kwa gari hili la kivita kunaashiria maendeleo ya kiteknolojia ya nchi hiyo, na kujitolea katika kuimarisha utayari wa kijeshi bila kujali chunguzi za na vikwazo.

Sifa za gari hii, kama vile bunduki yake yenye nguvu ya milimita 105 inayodhibitiwa kwa mbali, inaonyesha maendeleo ya kihandisi wa kijeshi nchini Korea Kaskazini, na umuhimu wake mikakati ya vita vya kisasa inayosisitiza uhamaji wa haraka na uzito wa mashambulizi.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya