ZINAZOVUMA:

Kituo cha biashara Afrika mashariki chajengwa Ubungo.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amehudhuria hafla ya uwekwaji wa jiwe...

Share na:

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 20, 2023 amehudhuria hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Kibiashara cha Afrika Mashariki, katika eneo la Ubungo ambacho kinajengwa na Kampuni ya East Africa Commercial and Logistics Center ya nchini China.

Mradi wa Kituo cha Kibiashara Afrika Mashariki unaojengwa katika eneo la Ubungo utakuwa na maduka 2060 yenye ukubwa wa jumla ya mita za mraba 75000 ambapo eneo hilo litakuwa na huduma zote za kibiashara ikiwemo mabenki na huduma ufungishaji na usafirishaji.

Mradi huo utazalisha ajira za moja kwa moja zaidi 15000 na utahamasisha maendeleo ya setka mbali mbali ambazo nazo zitazalisha ajira zisizo za moja kwa moja 50000 hivyo kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha kwa wananchi wa Tanzania.

Mapato ya jumla kwa mwaka yatafikia zaidi ya USD Milioni 500 mradi huo ukiwa umekamilika hivyo kusaidia katika ukuaji wa pato la Taifa la Tanzania na kuongeza mapato ya kikodi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya