Raisi wa Kenya William Ruto amesema kila raia wa Kenya atakua akichagia asilimia 3 ya mapato yake kwenye mfuko wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili kuwasaidia watu wengi zaidi kununua na kumiliki nyumba hizo.
Amesema wakati Serikali inapoanzisha mpango huo wa ujenzi lazima kuwe na mpango madhubuti unaolenga kushughulikia ufadhili wa watu wenye kipato cha chini.
Ruto amesema lengo la serikali ni kuongeza mapato katika mfuko wa hifadhi wa jamii wa Kenya ambao ndio utasaidia katika mradi wa ujenzi na kuisaidia nchi katika kuweka akiba.
Aidha hatua hiyo inaonekana kuwa ni njia mbadala ya kupunguza madeni kutoka mataifa ya magharibi na kuanza kutegemea vyanzo vya ndani vya mapato.