Makamu wa Raisi wa marekani Kamala Harris ameondoka nchini Tanzania baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu.
Kamala anaelekea nchini Zambia ambapo atamaliza ziara yake ya kiserikali barani Afrika.
Akiwa Tanzania amekutana na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam na kuzungumza mambo mbalimbali ikiwepo kuimarisha ushirikiano wa mataifa haya mawili na masuala ya kiuchumi.
Pia, viongozi hao wamezungumza namna Tanzania inavyofanya vizuri kuimarisha demokrasia, na kuinua wanawake kiuchumi. Pia Bi. Kamala amempongeza Rais Samia kwa hatua mbalimbali alizochukua ikiwemo kuruhusu mikutano ya hadhara na kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari.
Kamala amekuwa na takribani wiki moja ya ziara ya kikazi barani Afrika, ambapo ziara yake ilianzia Ghana.