ZINAZOVUMA:

JKCI kupokea wagonjwa wa Sierra Leone

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imepokea wageni kutoka...

Share na:

Ujumbe wa wataalamu wa Wizara ya Afya kutoka Sierra Leone, wameingia makubaliano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) uwatibu wagonjwa wa moyo kutoka Sierra Leone,

Wataalamu hao walikuja nchini kujifunza namna ya kuanzisha matibabu ya moyo nchini kwao, ambapo wlaishangazwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Tanzania katika Taasisi hiyo ya Moyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter Kisenge, amesema kuwa ziara hiyo inalenga kuendeleza ushirikiano wa matibabu ya moyo kati ya Tanzania na Sierra Leone, ikiwa ni dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutangaza utalii tiba kimataifa.

“Ujumbe huu umefika hapa nchini kujifunza uwekezaji wa matibabu ya moyo na usambazaji wa dawa na vifaa tiba kutoka kwa Bohari ya Dawa (MSD), ikiwa ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya Rais Dk. Samia,” amesema Dk. Kisenge.

Amesema ujumbe huo wa wataalamu kutoka Sierra Leone, umekiri kujifunza mambo mengi kutoka JKCI na wataleta wagonjwa, pamoja na kuazimia kwenda kuanzisha taasisi yao kwa ushirikiano na JKCI.

Dk. Kisenge amesema wataalamu hao pia wamejifunza utendaji kazi mkubwa na imara kutoka kwa watumishi wa JKCI, ikiwamo namna ya kuhudumia wagonjwa mahututi.

Ugeni huo ni hatua kubwa kwenye kutimiza malengo ya Rais Dk. Samia, katika kukuza utalii tiba nchini kutokana na uwekezaji mkubwa alioufanywa kwenye sekta ya afya.

Ameongeza kuwa, mbali na huduma za upasuaji wanazofanya hospitalini hapo, wanaendelea kutoa huduma za upimaji wa moyo kupitia mpango wa Dk. Samia wa Tiba Mkoba (Outreach) uliotangazwa na Wizara hivi karibuni.

Amesema mpango huo unasogeza huduma hizo karibu na wananchi huku wakizijengea uwezo hospitali zingine za kanda ikiwamo Benjamin Mkapa pia Chato na Geita.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya