ZINAZOVUMA:

Jeshi latangaza kuiongoza nchi Gabon

Mamlaka ya jeshi nchini Gabon imetangaza kumpindua Rais Ali Bongo...

Share na:

Maofisa wa Jeshi nchini Gabon wametangaza kuchukua mamlaka ya kuiongoza nchi hiyo katika kituo cha televisheni cha Taifa hilo, ikiwa ni siku chache tangu Uchaguzi mkuu ufanyike.

Pia wamesema wanafuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumamosi, ambapo Rais Ali Bongo alitangazwa mshindi.
Tume ya uchaguzi ilisema Bongo alishinda katika uchaguzi ambao upinzani ulidai kuwa ulikuwa wa udanganyifu.

Kupinduliwa kwa Bongo kunatamatisha uongozi wa familia yake iliyodumu kwa miaka 53 madarakani nchini Gabon.

Wanajeshi hao 12 walionekana kwenye televisheni wakitangaza suala hilo huku pia wakitangaza kufunga mipaka ya nchi hiyo.

“Tumeamua kulinda amani kwa kukomesha utawala uliopo,”amesema mmoja wa wanajeshi hao.

Ofisa huyo wa jeshi aliongeza kuwa sababu nyingine ni zilizowafanya kuchukua mamlaka ni pamoja na kuwepo kwa utawala usiowajibika, usiotabirika na kusababisha kuzorota kwa uwiano wa kijamii ambao unahatarisha nchi katika machafuko.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya