Usumbufu mkubwa wa umeripotiwa baada ya kukatika kwa mtandao wa intaneti katika mataifa mbalimbali barani Afrika.
Miongoni mwa nchi zilizotajwa katika ripoti hiyo ni Afrika Kusini, Nigeria, Ivory Coast, Liberia, Ghana na Burkina Faso. Taarifa hizo hazijasema sababu a nyaya za kusambaza huduma hiyo kushindwa kufanya kazi kwa kiwango kilichotarajiwa.
“Inaonekana kuna usumbufu wa mtandao, unaoathiri kutoka kaskazini hadi kusini mwa Afrika,” ilisema Cloudflare Radar, ambayo inatoa taarifa juu ya miunganisho ya mtandao.
Kasi ya muunganisho wa intaneti nchini Ivory Coast ulipungua hadi karibu 4% Alhamisi asubuhi, kulingana na Netblocks, ambayo inafuatilia usalama wa mtandao na muunganisho wa intaneti.
Nchini Liberia kasi ya muunganisho wakati mmoja ilishuka hadi 17% wakati Benin ilikuwa 14% na Ghana 25%, Netblocks ilisema.
Nchini Afrika Kusini, Vodacom ilisema kuwa “wateja kwa sasa wanakumbana na matatizo ya muunganisho wa mara kwa mara kutokana na kukatika kwa nyaya nyingi chini ya bahari”. Changamoto hii ya imetokea baada ya kukatika kwa mkongo wa kimataifa wa Intaneti baina ya Ulaya na Afrika Kusini kulingana na taarifa iliyotolewa na Vodacom Afrika Kusini kwenye ukurasa wa X (Twitter).