ZINAZOVUMA:

INDIA kununua mbaazi za Tanzania

Mama samia arudi kutoka India akiwa na uhakika wa soko...

Share na:

Mama Samia amemaliza ziara yake ya kitaifa ya siku 4 nchini India, ambapo amefanikiwa kuingia makubaliano mbalimbali.

Miongoni mwa makubaliano aliyofanikiwa kuweka kibindoni, ni ununuzi wa mbaazi tani laki 2 kutoka Tanzania.

Kwa muda mrefu wanunuzi wa mbaazi Tanzania, wamekuwa wakitoka India.

Hata hivyo wanunuzi hao walisitisha kununua mbaazi miaka michache iliyopita, na kusababisha soko la mbaazi kuporomoka nchini.

Kwa makubaliano haya ya nchi hizo mbili, soko la mbaazi linaweza kupanda kutokana na uhakika wa soko la zao hilo.

Kwani kwa mauzo hayo ya mbaazi nchi inaweza kujiingizia kipato kizuri tu, kutokana na mauzo ya takriban dola za marekani bilioni 400 kwa mwaka.

Mbali na mafanikio hayo, Mama Samia amefanikiwa kupata uhakika wa kutengenezwa kiwanda cha Matrekta, na tayari upembuzi yakinifu wa mradi huo umefanyika.

Na kwa mtazamo wa serikali, Mahindra wakishindwa kutengeneza kiwanda hicho, anaweza kukaribishwa muwekezaji mwingine kuendelea na mradi huo.

Pia zao la korosho ambalo limekuwa likinunuliwa na India kwa muda mrefu linaweza kuona mabadiliko, kwa kutengenezwa kiwanda cha korosho.

bado haijafahamika kitakuwa cha kubangua pekee au kitamalizia hatua nyingine na kutoa bidhaa kwa ajili ya mlaji.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya