Chuo cha Teknolojia kinachofahamika kama IIT nchini india, kimeanza kushika kasi ya kusambaza matawi yake duniani ikisaidiwa na IIT Madras na Delhi..
Chuo hicho kina matawi 23 nchini India, huku ikibebwa kwa umaarufu wa matawi ya ya IIT Delhi na IIT Madras.
Huku tawi la kwanza linalofahamika kama IIT Kharagpur, likiwa limeanzishwa mwaka 1951 katika jimbo la Bengali Magharibi.
Hii ni kutokana na mipango yake au kualikwa na nchi husika, ili lifunguliwa tawi la chuo hicho.
Chuo hicho kilifungua tawi lake nchini Zanzibar, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2023.
Tawi hilo linatarajiwa kuongozwa na mwanamama Preeti Aghalayam, ambaye pia amesoma shahada yake ya kwanza IIT-Madras.
Na anatarajiwa kuanza kudahili na kusomesha kozi mbili, katika tawi hilo la Zanzibar.
Kabla ya hapo tawi la Delhi la chuo hicho lilianza kufungua tawi lake, katika jiji la Abu Dhabi ndani ya Falme za Umoja wa Kiarabu.
Tawi hilo ndio la kwanza kuanzishwa na chuo hicho nje ya nchi ya India mwaka 2022.
Na sasa tayari kuna taarifa za chuo hicho kuitwa na serikali ya uingereza, kuanzisha tawi la chuo hicho.
Huku kukiwa na taarifa nyingine kuwa, Uingereza inaweka mipango ya kuwezesha vyuo vyake kuanzisha matawi nchini India.
Na katika kukazia hilo, Waziri mkuu wa india, Narendra Modi amesema kuwa tayari kuna nchi nyingi zimekuwa zikileta maombi ya chuo hicho kuanzisha tawi katika nchi zao.
Na kuongeza kuwa dunia imeona ipo haja ya kuchukua chachu ya kiteknolojia kutoka India.