Idara ya usalama nchini Ukraine (SBU) imesema kuwa imetibua njama ya kumuua Rais Volodymyr Zelensky iliyopangwa na Urusu na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa Ukraine.
Katika harakati hizo wamekamatwa maKanali wawili wa kitengo cha ulinzi wa serikali ya Ukraine, huku Idara hiyo ya Usalama ikisema kuwa maafisa hao wa jeshi ni mawakala wa kitengo cha usalama wa Serikali ya Urusi (FSB).
Inasemekana mawakala hao wa mtandao wa urusi walikuwa wakitafuta “watekelezaji” kutoka katika kundi la walinzi wa Rais Zelensky ili kumteka nyara na kumuua.
watu wengine waliolengwa najma za mtandao huo ni mkuu wa ujasusi wa kijeshi Kyrylo Budanov na mkuu wa SBU Vasyl Malyuk, iliongeza taarifa kutoka idara hiyo ya Usalama.
Kundi hilo liliripotiwa kupanga kumuua mkuu wa ujasusi wa kijeshi wa Ukraine Bw Budanov, kabla ya Pasaka ya Orthodox ambayo mwaka huu iliangukia tarehe 5 Mei.
Kulingana na SBU, kundi hilo lilikuwa linapanga kutumia msaliti wa kutokea ndani ili kupata habari za eneo alipo, abapo wangeshambulia kwa roketi na ndege zisizo na rubani.
Baadhi ya watu katika intelijensia wanasema kuwa taarifa ya kifo cha Zelensky ilipangwa kuwa zawadi ya kuapishwa kwa Putin kwa muhula wake wa 5 kama rais wa Urusi.