ZINAZOVUMA:

IDADI YA WAKONGO KUTAFUTA HIFADHI BURUNDI YAONGEZEKA

Share na:

Maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchini Burundi kujinusuru na mapigano yanayoendelea, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) likidokeza kwamba hali inazidi kuwa mbaya kutokana na upungufu wa rasilimali, hivyo kuagiza hatua za dharura zichukuliwe.

Kituo kipya cha kupokea wakimbizi cha Kansega katika eneo la Ndava, Mkoa wa Bujumbura karibu na mpaka wa DRC kimeanzishwa ili kusaidia raia wanaoingia kutafuta hifadhi.

Kati ya Desemba 5 na Desemba 11, UNHCR limesajili wakimbizi wapya 40,000 wa Kongo waliowasili Burundi. Wakimbizi hao wamegawanywa katika vituo vitatu vya mpito Kansega, Cishemere na Gatumba.

Hata hivyo, jana Alhamisi Desemba 11, 2025 iliripotiwa takribani raia wa Congo zaidi ya 200,000 waliyakimbia makazi kutokana na machafuko hayo.

Endelea Kusoma