Zaidi ya watu 186 wamefariki mpaka sasa kufuatia mapigano yanayoendelea Khartoum, Sudan kati ya jeshi la Sudan dhidi ya wanamgambo wa Rapid Support Force, RSF.
Takwimu zinaonesha Watu 1,800 wamejeruhiwa kutokana na mapambano hayo ya kuwania madaraka nchini humo.
Hali imezidi kuwa mbaya kufuatia mashambulizi ya siku tatu mfululizo huku umuoja wa nchi za Afrika ukipanga kutuma baadhi ya viongozi wa nchi jirani kuwa wapatanishi katika mzozo huo.