ZINAZOVUMA:

Franco apendekezwa katika Bodi ya Benki ya Ulaya

Serikali ya Italia imempendekeza Bw. Daniele Franco waziri wa zamani,...

Share na:

Kupitia waziri wa Uchumi wa Serikali ya Italia Bw. Giancarlo Giorgetti, Bw. Daniele Franco amependekezwa kushika nafasi katika bodi ya wakurugenzi ya Benki kuu ya Ulaya, ECB.

Nafasi hiyo inayotarajiwa kushikwa na Bw. Franco, inatarajiwa kuwa wazi mwezi wa kumi baada ya Bw. Fabio Panetta kuondoka katika bodi hiyo.

Sababu inayomtoa bw. Panetta katika bodi hiyo, ni maandalizi ya kuanza kazi yake mpya kama gavana wa Benki ya Italia.

Maamuzi hayo yamewashangaza wengi, lakini inaonesha ni maamuzi yaliyoafikiwa na serikali nzima ya waziri mkuu wa sasa, Giorgia Meloni.

Bwana Franco mwenye umri wa miaka 70, ni katika wachumi wenye uwezo mkubwa nchini Italia, na amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo Gavana wa Benki ya Italia na mkaguzi wa hesabu za Serikali.

Alichaguliwa kuwa Waziri wa Uchumi mwaka 2021 akiisaidia Italia kushinda vita ya kiuchumi wakati wa Uviko 19 na hali mbaya iliyosababishwa na Urusi baada ya kuivamia Ukraine.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya