Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) inayosimamia Ulinzi wa Taarifa Binafsi kutoka Nchini Ireland (DPC) imechukua uamuzi wa kuipiga faini ya Trilioni tatu kampuni ya META.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya kampuni ya META kukiuka agizo la kutohamisha data za watumiaji wa Facebook kwenda Marekani.
DPC ilitoa miezi 5 kwa META kusitisha uhamishaji wa Taarifa Binafsi za Watumiaji wake ikiwa ni utekelezaji wa zuio la Mahakama ya EU lililotolewa mwaka 2020 dhidi ya kampuni zinazochakata na kuhifadhi TaarifaBinafsi.
Hadi sasa, META imefikisha faini za Tsh. Trilioni 5.9 kutokana na ukiukaji wa Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa data ya Umoja wa Ulaya (GDPR), iliyoanzishwa mwaka wa 2018.