Raisi wa klabu ya Yanga Eng. Hersi Said ateuliwa kushika nafasi ya mwenyekiti wa chama kipya cha Muungano wa klabu za Afrika (ACA).
Eng. Hersi ameteuliwa kushika nafasi hiyo kupitia mkutano ulofanyika, jijini Cairo nchini Misri siku ya Alhamisi.
Mkutano huo uliojumuisha viongozi wa vilabu vya soka takriban 60 kutoka afrika, huku Dr. Patrice Motsepe akiwa mwenyeji wa mkutano huo.
Huku Tanzania ikiwakilishwa na Eng. Hersi Said Aliyepata uenyekiti, pamoja na Salim Abdallah ‘Try Again’ mwenyekiti wa bodi ya Simba.