ZINAZOVUMA:

Dkt. Magembe: Tutumie Ardhi vizuri

Dkt. Magembe awaasa watanzania kutumia ardhi vizuri katika ujenzi wa...

Share na:

Mhadhiri mwandamizi Dkt. Dawa Magembe kutoka Chuo Cha Ardhi, ameishauri jamii ya watanzania, kuacha matumizi holela ya ardhi na badala yake kutumia wataalamu wa ardhi ili kuyapa thamani makazi yao.

Muhadhiri huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishiwa, katika maonesho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika shule ya Popatlal iliyopo Jijini Tanga.

Mhadhiri huyo aliendeleakwa kusema kuwa ujenzi wa nyumba kiholela hupelekea athari mbalimbali za mabadiliko ya tabianchi kimazingira,kiuchumi na kijamii.

“Ujenzi holela unapelekea athari nyingi za kimazingira, kwani husababisha kuleta madhara yanayo tokana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwanza ujenzi holela huziba maeneo ya asili ya kupitisha maji, pili husababisha madhara makubwa ikitokea ajali ya moto kwa kuzuia magari kufika eneo la tukio, lakini pia unasababisha maisha kuwa duni na kupeleke mali husika mfano nyumba kushuka thamani”

Aidha Dkt. Magembe alisema kuwa kwa sasa chuo cha Ardhi kinaendelea na miradi mbalimbali ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi, ambapo jijini Tanga wanapanga fukwe ili ziweze kufuata kanuni za kimazingira na kuweza kutumika na watu wa rika zote na salama kwa ajili ya mapumziko.

Pia Jijini Tanga chuo hicho kimebuni mradi wa makazi endelevu karibu na bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga, kwa kuzingatia upangaji wa matumzi bora ya ardhi.

Hata hivyo amesema kuwa miradi yote inayo buniwa hushirikisha viongozi mbalimbali wa Halmashauri na hufanyika kwa uhalisia ili iweze kutekelezwa na kuwasaidia wananchi.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya