ZINAZOVUMA:

CRDB yamwaga mabilioni kunogesha Mapinduzi Cup

CRDB knogesha Mapinduzi Cup kwa kumwaga bilioni 3.7 kwa miaka...

Share na:

Benki ya CRDB nchini Tanzania imesaini mkataba wa kudhamini kombe la Mapinduzi Cup kwa zaidi ya shilingi bilioni 3.7. Udhamini huo ni wa miaka mitatu kulinganana mkataba uliosainiwa hapo jana.

Mkataba huo wa udhamini ulisainiwa jana kati ya Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania Wallace Karia na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Abdulmajid Nsekela. Kombe hilo lililokuwa likifahamika kama Azam Sports federation Cup, litafahamika rasmi kama CRDB Bank Federation Cup.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw. Abdulmajid Nsekela amesema kuwa benki yake itatoa dola za marekani laki moja sawa na milioni 225 kwa TFF ili kumalizia mechi zilizobaki msimu huu.

Nakuongeza kuwa kwa msimu wa mwaka 2024/2025 TFF itapokea milioni 800, na msimu 2025/2026 watapokea bilioni 1 na watamaliza mkataba msimu wa 2026/2027 kwa kupokea bilioni 1.2. Fedha hizo zitajumuisha zawadi kwa bingwa wa ligi hiyo, mchezaji bora kila mechi, mchezaji bora wa mashindano yote, goli bora la mechi, goli la msimu na timu bora ya msimu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya