ZINAZOVUMA:

Buriani, Edward Lowassa watanzania watakukumbuka kwa ujasiri wako

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa (70) amefariki dunia,...

Share na:

Imeandaliwa na Selemani Magali

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Edward Lowassa (70) amefariki dunia, akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.

Tangazo la kifo cha Lowassa kimetangazwa Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Philip Mpango.

Katika tangazo fupi alilolitoa kupitia televisheni ya taifa, Mpango amesema kuwa Lowassa amefikwa na umauti katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Lowassa alihudumu kama Waziri Mkuu wa Tanzania chini ya Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa miaka mitatu, toka 2005 mpaka 2008 alipolazimika kujiuzulu kufuatia kashfa ya Richmond.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia hii leo.

Mwaka 2015 Lowassa alikihama chama tawala cha CCM baada ya kukosa tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho. Alitimkia chama kikuu cha upinzani cha Chadema ambapo aliungwa mkono kugombea urais na vyama vilivyounda umoja wa upinzani wa UKAWA kwa wakati huo.

Lowassa hata hivyo alishindwa katika uchaguzi huo na aliyekuwa mgombea wa CCM John Pombe Magufuli. Lowassa alirejea CCM mwaka 2019.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya