ZINAZOVUMA:

BILIONEA WA KIARABU AAHIDI MAMILIONI KWA KIPCHOGE

Eliud kipchoge

Share na:

Mjadala mkubwa umeibuka mitandaoni baada ya kusambaa kwa chapisho linalodai kuwa bilionea wa Saudi Arabia Sheikh Khalid bin Al-Fahad, amempa ofa nono bingwa wa marathon duniani, Eliud Kipchoge, ikiwa atabadili uraia na kuwakilisha Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, bilionea huyo anadaiwa kumwambia Kipchoge kuwa ametelekezwa na taifa lake la Kenya, huku akimwahidi dola bilioni moja taslimu pamoja na dola milioni 500 kila mwaka endapo atakubali kubadili uraia na kushiriki mashindano chini ya bendera ya Saudi Arabia.

Mbali na malipo hayo atakayopewa, Kipchoge ameahidiwa pia kujengewa uwanja mkubwa jangwani, utakaopewa jina la Kipchoge Desert Dome, wenye siti elfu 80 katika jiji la Riyadh.

Taarifa hiyo imezua mjadala mkali katika ulimwengu wa michezo na mitandao ya kijamii, huku wengi wakijadili masuala ya uzalendo, heshima ya wanamichezo waliolitumikia taifa lao kwa muda mrefu, pamoja na kuongezeka kwa ushawishi wa fedha kubwa katika michezo ya kimataifa.

Hadi sasa, hakuna tamko rasmi kutoka kwa Eliud Kipchoge, serikali ya Kenya wala mamlaka za michezo za Saudi Arabia kuthibitisha au kukanusha madai hayo, lakini sakata hilo limeendelea kuchochea mjadala mpana kuhusu nafasi ya wanamichezo katika zama za nguvu ya mitaji mikubwa.

Endelea Kusoma