Licha ya serikali kuvifunga viwanda viwili vya kuchinja nyama ya punda katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma, imebainika biashara ya mnyama huyo bado inaendelea kufanyika kinyemela.
Hatua hiyo inatishia kuhatarisha kutoweka kwa mnyama huyo endapo hatua za kusitisha hazitachukuliwa.
Mkuu wa programu kutoka shirika la IFTz, linalojihusisha na maendeleo ya wakulima, Uchumi na ustawi wa jamii, Jacqueline Nicodemus, amesema pamoja na serikali kuvifunga viwanda vya nyama ya punda na kupiga marufuku biashara ya nyama, ngozi na uchinjaji lakini bado biashara hiyo inaendelea kufanyika kinyemela.
Amesema shirika la IFTz kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine bado linaendelea kukabiliana na kudhibiti vitendo vya kuchinja punda.