ZINAZOVUMA:

Bi Mapisa, Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za Rushwa

Spika wa Bunge la Afrika Kusini kwa sasa na waziri...

Share na:

Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula amejiuzulu baada ya polisi kuvamia nyumba yake wakichunguza tuhuma ya rushwa.

Bi Mapisa-Nqakula anatuhumiwa kuitisha hongo ili kupeana kandarasi wakati alipokuwa waziri wa ulinzi.

Amekana mashtaka na kusema kujiuzulu kwake hakumaanishi kukubali hatia na alisema kutokana na uzito wa uchunguzi hawezi kuendelea na jukumu lake.

Bi. Mapisa-Nqakula mwenye umri wa miaka 67 na mwanaharakati mkongwe wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi aliteuliwa kuwa spika mwaka wa 2021 kabla ya hapo, alihudumu kama waziri wa ulinzi kwa miaka saba.

Wiki iliyopita mawakili wa Mapisa-Nqakula waliwasilisha ombi la kutaka amri ya mahakama izuie kukamatwa kwake, wakisema ingevunjia heshima yake.

Bi Mapisa-Nqakula anashtakiwa kwa madai kadhaa ya kuomba hongo ya kiasi cha dola za marekani 120,000, kutoka kwa mmiliki wa kampuni ili kupata zabuni ya kusafirisha vifaa vya jeshi nchini Afrika Kusini kutoka maeneo mbalimbali barani Afrika, gazeti la Business Day linaripoti.

Kujiuzulu kwake kumekuja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi ujao, ambao baadhi wanaamini unaweza kuwa mgumu kwa chama tawala cha African National Congress (ANC).

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya