Katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 iliyosomwa na waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba,kuna ongezeko la bilioni 3 zaidi ya bajeti iliyopita.
Huku Trilioni 34.4 kati ya trilioni 47.4 zitatokana na vyanzo vya ndani, michango ya wahisani ikiwa trilioni 4.29 na mikopo kwa ujumla wake ikiwa trilioni 8.69.
Mapendekezo hayo yanategemea kupata mikopo ya ndani ya trilioni 6.14, na mikopo ya nje trilioni 2.55.
Mbali na mapendekezo hayo, wizara ya fedha imependekeza kuweka sera za kupunguza matumizi ya fedha taslimu katika miamala ya kila siku nchini, kurasimisha biashara za kutoa mikopo midogo ya kati, pamoja na kuanzisha tuzo ya uzalendo katika mfumo wa risiti za “EFD.”.
Pia serikali ina mpango wa kukuza ushiriki wa sekta binafsi katika biashara na uwekezaji, huku ikijitahidi kupunguza athari za majanga mbalimbali katika biashara na uwekezaji huo.