Nchi nne za G20 Brazil, Ujerumani, Hispania na Afrika Kusini zaridhia na kutia saini katika mkataba wa Kodi ya haki kwa matajiri wakubwa duniani.
Nchi hizo zimetia saini kwenye mkataba huo unaotaka matajiri duniani, wakatwe asilimia 2 ya utajiri wao, ili kuongeza ukwasi wa kupambana na majanga na maafa yanayotokea duniani kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Na kushawishi nchi nyingine kuunga mkono uamuzi wao kwa kusema kuwa, kodi hiyo ikianza kukusanywa pato la mwaka lingetosha kuhudumia maafa yote yaliyotokea mwaka jana kwa sababu za hali ya hewa.
Duniani kuna mabilionea karibu elfu 3, na kila mmoja akitoa asilimia 2 ya pato lake kama kodi hiyo, inaweza kukusanywa zaidi ya pauni bilioni 250 sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni 800 za kitanzania.
Nchi hizo pia zimeweka bayana kuwa ikiwa kodi hiyo itaanza kukuanywa itasaidia kuongeza usawa baina ya watu duniani, kuongeza ukwasi wa kupambana na majanga ya mlipuko, mabadiliko ya tabia nchi na hata mapigano ya kijeshi yanayoendelea Ulaya na Mashariki ya Kati.
Nchi ya Brazil ndio iliibeba ajenda hii ya kodi ya asilimia 2 ya pato kwa matajiri, na kuipeleka katika kikao Mawaziri wa Fedha wa G20 mwanzoni mwa mwaka huu.
Mbali na nchi hizo nne zilizosaini mkataba huo, pia Ufaransa na marekani zimeonyesha kukubali kodi kwa matajiri ingawa hawajakubali hoja ya kodi hiyo kuwa ya dunia nzima.