Mwanaume wa kwanza kupandikizwa figo iliyobadilishwa vinasaba kutoka kwa nguruwe ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 62 aliruhusiwa kwenda nyumbani, wiki mbili baada ya upasuaji wa dharura katika Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH).
Upandikizaji wa viungo kutoka kwa nguruwe waliobadilishwa vinasaba haukufanikiwa siku za nyuma.
Lakini mafanikio ya utaratibu huu hadi sasa yamesifiwa na wanasayansi kama hatua ya kihistoria katika uwanja wa upandikizaji.
Katika taarifa, hospitali ilisema mgonjwa, Richard Rick Slayman wa Weymouth, Massachusetts, alikuwa akipambana na ugonjwa wa figo na alihitaji kupandikizwa kiungo hiyo ili kuokoa maisha yake.
Madaktari wake walifanikiwa kufanya upandikizaji huo katika upasuaji ulifanyika kwa saa nne tarehe 16 mwezi Machi.
Walisema figo ya Bw Slayman sasa inafanya kazi vizuri na kwamba hahitaji kufanyiwa tiba ya dialysis.