ZINAZOVUMA:

Al Shabab washambulia SYL Hotel karibu na Ikulu

Kikundi cha wapigananiji wa Al Shabab nchini Somalia kimeshambulia hoteli...

Share na:

Wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al Shabab Alhamisi walishambulia hoteli maarufu karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, vyanzo vya usalama na mashahidi walisema.

Shambulio hilo ambalo al Shabab ilidai kuhusika, lilianza nyakati za saa tatu na dakika 45 usiku, wakati watu wenye silaha walipovamia hoteli ya SYL kwa risasi nyingi.

“Watu wengi wenye silaha waliingia kwa nguvu ndani ya jengo hilo baada ya kuharibu ukuta wa pembeni kwa mlipuko mkubwa,” Afisa Usalama Ahmed Dahir aliiambia AFP.

Haikufahamika mara moja ikiwa kuna vifo vilitokea.

Mashahidi walielezea kusikia washambuliaji wakifyatua risasi hovyo.

“Sina taarifa kuhusu majeruhi lakini kulikuwa na watu wengi ndani wakati shambulio hilo lilipoanza,” alisema Hassan Nur ambaye alitoroka kwa kupanda ukuta.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya