Akaunti ya mtandao wa ‘Facebook’ wa banki ya Zambia imedukuliwa na kubadilishwa picha yake ya utambulisho na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano wa (BOZ) aliyethibitisha kudukuliwa kwa akaunti hiyo, amewataka Wananchi kutojibu ujumbe wowote utakaotumwa kutoka kwenye akaunti hiyo hadi hapo Umma utakapoarifiwa kurejeshwa kwake.
BOZ imesema “Tunasikitika kuufahamisha umma kuhusu tukio la udukuzi wa mtandao ulioathiri ukurasa wa Facebook wa Benki Kuu. Tunafanya uhakiki wa kina kwa kushirikiana na Vyombo vya Sheria ili kuhakikisha kuwa sauala hili linashughulikiwa.”
Hata hivyo, Serikali imewahakikishia wananchi kuwa tukio hilo haliathiri ulinzi na usalama wa taarifa binafsi za fedha za wateja kwa sababu mifumo mikuu ya Benki Kuu haijadukuliwa na iko salama.