Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA) umeshinda tuzo ya Uwanja Bora wa Ndege Barani Afrika unaotoa huduma bora kwa abiria chini ya milioni mbili kwa mwaka (Best Airport Under 2 Million Passengers in Africa, zinazotolewa na Baraza la Kimataifa la Viwanja vya Ndege (Airport Council International – ACI).
Tuzo za kila mwaka za Huduma Bora za Viwanja vya Ndege (Airport Service Quality –ASQ) za ACI zinatambua ubora wa uwanja wa ndege kupitia maoni ya abiria kote duniani yanayopatikana kwa tafiti maalumu zinazofanywa kila siku kwa abiria katika maeneo wanayo ondoka (departure) na kuwasili(arrivals) katika vipengele mbalimbali ikiwemo Utendaji Bora wa Wahudumu (Most Dedicated Staff), Wepesi wa Safari kwa abiria (Easiest Airport Journey), Huduma zenye kukidhi matakwa ya mteja (Most Enjoyable Airport) na Usafi wa Majengo ya Abiria (Cleanest Airport).
ZAA ilijiunga rasmi na kuwa mwanachama wa ACI mnamo Oktoba 2022 kwa madhumuni ya kujipima huduma zake kwa abiria katika kipengele cha abiria wanaondoka /ASQ-eparture program) kwa watendaji wake (customer services agents) kupatiwa mafunzo rasmi na baraza hilo ambapo ilianza kupata matokeo bora zaidi ya ujumla kuanzia robo ya kwanza ya mwaka 2023 kwa kuwa namba tano kwa utoaji wa huduma kati ya Viwanja 17 vya Ndege Barani Afrika.
Mamlaka inatarajia kukabidhiwa rasmi tuzo hiyo mnamo tarehe 25 Septemba 2024 katika Mkutano na Maonyesho ya Kila Mwaka ya Huduma kwa Wateja Duniani (World’s Annual Customer Experience Summit and Exhibition) yatakayofanyika huko Atlanta nchini Marekani.