ZINAZOVUMA:

53 wateketea kwa moto Hawaii

Raisi wa Marekani Joe Biden ametangaza hali ya maafa baada...

Share na:

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza hali ya maafa huko Hawaii, ambapo moto mkali umeharibu kisiwa cha kitalii kilichopo katika mji huo na kuua takriban watu 53.

Idadi ya vifo vilivyosababishwa na moto huo mkali na kukaribia kuteketeza mji wa huo wa kitalii imefikia takriban watu 53 na huenda ikaongezeka, na kuifanya kuwa moja ya maafa mabaya zaidi katika historia ya jimbo hili la Marekani.

Sababu ya maafa hayo imetajwa kuwa ni moto uliochochewa na upepo mkali, unaosababishwa na Kimbunga Dora ambacho kwa sasa kinapita katika Bahari ya Pasifiki.

Gavana wa Jimbo hilo Josh Green amesema kuwa janga hilo ni kubwa zaidi la asili katika historia ya jimbo la Hawaii na limetokana na hali ya majira ya joto yaliyo na mfululizo wa matukio mabaya ya hali ya hewa duniani.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya