ZINAZOVUMA:

12 wafariki Congo kwa maporomoko ya udongo

Zaidi ya wakazi 12 wa eneo la Dibaya Lubwe wamefariki...

Share na:

Takriban watu 12 waliuawa na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo, baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi kwenye mto Kasai siku ya jumapili.

Mto Kasai unapatikana kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maporomoko hayo yalitokea Jumamosi adhuhuri katika wilaya ya Dibaya Lubwe katika jimbo la Kwilu, na kusababisha udongo na uchafu kwenye ukingo wa Mto Kasai.

Pia pembezoni mwa mto huo kulikuwa na watu wanafua na boti moja ilikuwa ikitia nanga.

Kaimu gavana wa jimbo hilo Felicien Kiway alisema, miili 12 imetolewa kutoka kwenye kifusi hadi sasa, ikiwa ni wanawake tisa, wanaume watatu na mtoto mchanga mmoja.

Pia taarifa ya Arsene Kasiama, Mratibu wa jumuiya ya Kiraia alisema kuwa maporomoko hayo ya udongo yaliwaangukia watu wengine waliokuwa kwenye harakati za manunuzi sokoni.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya